Sport
Dollar
38,1188
0.08 %Euro
43,4762
0.99 %Gram Gold
4.014,2000
1.49 %Quarter Gold
6.511,6500
0 %Silver
39,6800
0.21 %Picha mjongeo zilionesha magari ya kivita ya Israeli yakivunja sanamu katika mji wa Yaroun.
Jeshi la Israeli limevunja sanamu ya Mtakatifu George wakati Wakristu wa kusini mwa Lebanoni wakiwa wanasheherekea Jumapili ya Matawi.
Kulingana na chombo cha habari cha taifa la Lebanon (NNA), sanamu hiyo iliharibiwa siku ya Jumapili katika mji wa mpakani wa Yaroun.
"Picha mjongeo zimeonesha magari ya kivita yakivunja sanamu hiyo,” kilisema chombo cha habari cha Lebanon.
Waziri wa kazi wa zamani wa Lebanon Moustafa Bayram, aliweka picha hiyo kwenye ukurasa wake wa X.
“Bila aibu, jeshi la Israeli lilirekodi tukio hili, likionesha kusudio lao la kuendeleza udhalimu wao," alisema.
Hata hivyo, hapakuwa na tamko lolote kutoka kwa jeshi la Israeli kuhusiana na tukio hilo.
Wakristu wote ulimwenguni huadhimisha siku ya Jumapili ya Matawi kama kumbukumbu ya Yesu Kristo kuingia Yerusalemu, akijiandaa na mateso yake, kifo chake na kufufuka kwake, kulingana na imani ya Kikristo.
Comments
No comments Yet
Comment