Dollar

38,2612

0.13 %

Euro

43,8713

-0.48 %

Gram Gold

4.214,3700

0.12 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Ni katika ziara yake ya kiserikali ya siku nne nchini humo, ambapo mbali na hiyo, pia atajadiliana masuala mbalimbali ya kitaifa na kimataifa na mwenyeji wake Xi Jinping.

Rais Ruto kuongoza kongamano la biashara nchini China

Taarifa rasmi ya Serikali ya Kenya inasema, kiongozi huyo kutoka Afrika Mashariki atafanya mazungumzo na mwenzake wa China Xi Jinping ambapo viongozi hao wawili watazungumzia vipaombele vya pamoja katika kuleta mageuzi ya kiuchumi, maendeleo endelevu na ushirikiano wa kimataifa.

Ziara yake ni kati ya tarehe 22 hadi 26 Aprili 2024.

Rais Ruto pia anatarajiwa kuongoza Kongamano la Biashara kati ya Kenya na China, ambalo litaleta pamoja zaidi ya makampuni 100 kutoka nchi mbili hizo kwa lengo la kutafuta fursa mpya za kibiashara, uwekezaji, uvumbuzi wa kidijitali na ukuaji wa viwanda.

Katika ziara hiyo ya siku mbili, Rais Ruto pia atazindua Kituo cha Kumiliki Chai cha Kenya katika Mkoa wa Fujian na atatoa hotuba kuu katika Chuo Kikuu cha Peking, ambapo ataangazia maono ya Afrika ya ukuaji jumuishi, uongozi, na ushirikiano wa kina wa Kusini-Kusini.

Akiwa mwenyekiti wa sasa Jumuia ya Afrika Mashariki, atakuwa na majadiliano ya Amani na usalama katika eneo la Pembe ya Afrika na Ukanda wa Maziwa Makuu.

Ziara hii imetokea baada ya Rais wa China Xi Jinping kuendelea na shughuli zake za kidiplomasia kwa nchi zinazoendelea na kutafakari upya kuhusu misaada ya kigeni baada ya msukumo wa ushuru baina ya China na Marekani ulioanzishwa na Rais wa Marekani Donald Trump.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#