Dollar

38,2627

0.13 %

Euro

43,8789

-0.46 %

Gram Gold

4.222,9400

0.32 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Kenya imekumbwa na sakata la baadhi ya mashirika ya afya kutoa baadhi ya viungo vya miili ya watu kwa ahadi ya kuwalipa.

Serikali ya Kenya yaonya maafisa wa afya dhidi ya ukiukaji wa maadili

Waziri wa Afya nchini Kenya Aden Duale ametoa onyo kali kwa Baraza la Madaktari na Madaktari wa Meno nchini Kenya (KMPDC) dhidi ya kutoa leseni kwa vituo vya matibabu visivyo na sifa na visivyofuata sheria.

Amesisitiza kwamba afisa yeyote atakaekiuka sheria au usajili na kuhusika na utovu wa nidhamu atakabiliwa na hatua kali.

"Haitakuwa biashara kama kawaida," Duale amesema.

Alisema hayo katika ziara yake ya kwanza katika ofisi za KMPDC jijini Nairobi.

Tahadhari yake inakuja huku nchi hiyo ikikumbwa na sakata la mashirika kutoa sehemu za viungo vya miili ya watu kwa ahadi ya kuwalipa.

Wiki iliyopita huduma za upandikizaji figo katika hospitali ya Mediheal mjini Eldoret zilisitishwa kufuatia madai ya utovu wa nidhamu na ukiukaji wa maadili.

Maafisa wawili wakuu wa Wizara, Dkt Maurice Wakwabubi na Dkt Everlyne Chege, pia wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi.

Madai hayo ni pamoja na biashara ya viungo, ambapo figo ziliripotiwa kuvunwa kutoka kwa wafadhili chini ya mazingira ya kutiliwa shaka na kuuzwa nje ya nchi.

“Jukumu kuu la Baraza ni kuhakikisha Wakenya wote, bila kujali umri au hali ya kiuchumi, wanaweza kupata huduma salama za afya zinazotolewa na wataalamu waliohitimu,” Duale aliongezea.

Waziri alilitaka Baraza hilo kuzingatia uadilifu, uwazi, na huduma kwa umma kama ilivyoainishwa chini ya Kifungu cha 33(2) cha Sheria ya Bima ya Afya ya Jamii ya 2023.

"Acheni shughuli zenu ziakisi uadilifu, uwazi, na huduma kwa umma," alihimiza, huku akitoa wito wa utoaji wa huduma kwa wakati, kazi ya pamoja, na matumizi bora ya rasilimali za umma.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#