Sport
Dollar
38,4187
0.2 %Euro
43,6777
-0.22 %Gram Gold
4.070,5100
-1.43 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Kundi lenye ushirikiano na al-Qaeda limedai kuvamia kambi ya Wargaadhi, lakini Wizara ya Ulinzi ya Somalia inakanusha hilo na kusema kuwa bado kambi hiyo iko chini ya udhibiti wa jeshi la taifa
Kundi la kigaidi la al-Shabaab siku ya Alhamisi lilifanya mashambulizi ya kushtukiza alfajiri katika kambi moja muhimu ya jeshi la Somalia kwenye kijiji cha Wargaadhi kilichoko katika jimbo la kusini kati la Hirshabele, na kusababisha mapigano makali.
Kulingana na afisa mmoja wa usalama aliyezungumza na shirika la habari la Anadolu kwa njia simu lakini jina halikutambulishwa kwa sababu za kiusalama, Jeshi la Somalia, likisaidiwa na wapiganaji wa eneo hilo, walikabiliana vikali na kundi hilo linaloungwa mkono na al-Qaeda, na kusababisha vifo kwa pande zote mbili.
Licha ya madai ya al-Shabaab kuwa imeteka vijiji na kuchukua udhibiti wa kambi hiyo ya jeshi, Wizara ya Ulinzi ya Somalia inasema Wargaadhi bado iko chini ya usimamizi wa jeshi.
“Wargaadhi bado inadhibitiwa kikamilifu na jeshi la Somalia na vikosi vya eneo hilo,” wizara ilisema katika taarifa.
Wargaadhi ni kambi ya jeshi ya pili kwa ukubwa katika kanda ya Shabelle, baada ya mji muhimu wa Adan Yabaal, ambao pia ulikuwa umedhibitiwa na al-Shabaab.
Kijiji hiko ni muhimu sana kimkakati kwa kuwa kinaunganisha kambi za jeshi za Eel-Dheer na Masagaway katika jimbo la kati la Galmudug.
Kundi la al-Shabaab limezidisha mashambulizi yake dhidi ya vikosi vya serikali ya Somalia na maeneo muhimu ya kijeshi katika sehemu ya kati tangu kuanza kwa Ramadhan mwezi uliopita.
Comments
No comments Yet
Comment