Dollar

38,4254

0.22 %

Euro

43,7140

-0.14 %

Gram Gold

4.089,8900

-0.96 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Jeshi linasema limedhibiti kambi za mwisho za mafunzo ambazo bado zilikuwa zinatumiwa na waasi katika mkoa wa kaskazini mwa nchi wa Cabo Delgado.

Msumbiji yatangaza kumalizika kwa uasi katika mkoa wenye utajiri wa gesi wa Cabo Delgado

Siku ya Alhamisi Msumbiji imetangaza kudhibiti kambi za mwisho za mafunzo zilizokuwa zikitumiwa na waasi katika mkoa wake wa kaskazini wa Cabo Delgado, ishara ya kile maafisa wanakitaja kuwa kumalizika kwa uasi wa miaka mingi.

Mkuu wa Ujasusi wa jeshi Ricardo Macuvele alisema operesheni hiyo ilifanikiwa kutokana na mchango wa vikosi vya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika nchini Msumbiji, ambavyo vilichangia zaidi katika kuwashinda waasi.

Kiwango kikubwa cha gesi asilia kiligunduliwa katika eneo la Cabo Delgado 2010. Wapiganaji wanaohusishwa na kundi la DAESH walianzisha uasi sehemu hiyo 2017, na kusitisha uchimbaji wa gesi hiyo iliyogunduliwa 2010. Karibu watu 5,800 wameuawa.

Kampuni ya TotalEnergies, ambayo ilisitisha mradi mkubwa wa gesi baada ya mashambulizi ya 2021 ambapo watu kadhaa waliuawa, ilisema mapema kuwa mradi wa gesi mwaka huu utaanza tena pale "amani na usalama" itakaporejea Cabo Delgado.

‘Kudhibiti hali’

"Zambia pia ilisaidia pakubwa katika kudhibiti hali, eneo ambalo mlitusaidia kulidhibiti kutoka kwa magaidi; bado tunalisimamia na tumefanikiwa kudhibiti hata kambi za mwisho ambazo waasi walikuwa wanatumia kwa mafunzo," alisema Macuvele katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya Ulinzi ya Zambia siku ya Alhamisi.

Macuvele aliyasema hayo wakati wa ziara yake katika mji mkuu wa Zambia, Lusaka, ambapo alikutana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi ya Zambia Maambo Haamaundu.

Haamaundu amesema Zambia iliungana na majirani zake katika kukabiliana na ugaidi na uhalifu unaovuka mipaka, ikiwemo usafirishaji haramu wa watu.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#