Sport
Dollar
38,1588
0.3 %Euro
43,6101
1.61 %Gram Gold
3.958,7400
2.25 %Quarter Gold
6.529,2600
2.67 %Silver
39,4700
3.6 %Serikali ya Waziri Mkuu Navin Ramgoolam imeituhumu serikali iliyopita ambapo maafisa wawili wa zamani wanadaiwa kughushi takwimu za uchumi.
Mamlaka nchini Mauritius imemkamata aliyekuwa waziri wa fedha na gavana wa benki kuu Jumatano kama sehemu ya uchunguzi wa matumizi mabaya ya fedha katika kampuni ya serikali, imesema Kamisheni ya Taifa ya Uhalifu wa fedha.
Gavana wa zamani wa benki kuu Harvesh Seegolam na aliyekuwa waziri wa fedha Renganaden Padayachy wamekana tuhuma hizo na walikataa kulizungumzia suala hilo.
Serikali ya Waziri Mkuu Navin Ramgoolam imeituhumu serikali iliyoondoka madarakani na viongozi hao wawili kwa kutoa takwimu za uongo za ukuaji wa uchumi, upungufu wa bajeti na deni la taifa kwa miaka mingi.
Katika hatua yake ya kwanza baada ya kuchaguliwa kuingia madarakani Novemba mwaka jana, Ramgoolam alianzisha ukaguzi wa mahesabu ya umma. Hii sio mara ya kwanza kwa gavana wa zamani kukamatwa.
“Renganaden Radayachy na Havesh Seegolam wamekamatwa jioni hii kufuatia ushahidi mpya ulioletwa wa tuhuma za ubadhirifu wa repee za Mauritius milioni 300 ($6.70 milioni), imesema kamisheni ya uhalifu wa fedha.
Uchunguzi wa ubadhirifu unahusishwa na tuhuma za wizi wa fedha kutoka Shirika la Uwekezaji la Mauritius, lililoundwa kusaidia kampuni kupambana na athari za janga la Uviko.
Comments
No comments Yet
Comment