Sport
Dollar
38,1588
0.3 %Euro
43,6101
1.61 %Gram Gold
3.958,7400
2.25 %Quarter Gold
6.529,2600
2.67 %Silver
39,4700
3.6 %Mamlaka zinalaumu ajali hiyo kwa wahusika kushindwa kuheshimu utaratibu wa kuendesha chombo, ikiwemo kujaza abiria zaidi ya kiwango kinachotakiwa kutokuwa na ufahamu wa muelekeo wakati wa usiku.
Watu zaidi ya 50 wamekufa na wengine wengi hawajulikani waliko baada ya boti lililokuwa limejaa watu kupindukia katika mto mkoa wa Equateur, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, televisheni ya taifa iliripoti siku ya Alhamisi.
Boti hiyo ilikuwa imebeba karibu abiria 100 wakati ilipozama katika Mto Congo usiku wa kuamkia Jumanne, karibu na Mayita, mji ulioko takriban kilomita 40 kutoka mji wa Mbandaka.
“Watu zaidi ya 50 wamefariki” ni idadi ambayo tumeipata kwa haraka kufikia sasa, Maitre Kolomba Mampunia, msimamizi wa shirika la Msalaba Mwekundu wa mkoa wa Equator, ameiambia televisheni ya taifa RTNC.
Sehemu ya juu kuanguka
Boti hilo, lenye jina la Fortune HB Jado, lilikuwa linaelekea katika soko ya Mobenzani eneo la Bomongo kutoka mji wa Mbandaka, wakati sehemu ya juu ilipoanguka wakati boti ikijaribu kutia nanga, kulingana na taarifa.
Mboyo Loyoko, kamishna wa mto huo, amesema ajali hiyo imetokana na wahusika kutozingatia utaratibu wa kuendesha chombo, ikiwemo kujaza abiria zaidi ya idadi inayotakiwa na kutokuwa na ufahamu wa muelekeo wakati wa usiku.
Gavana wa Equateur, Bobo Boloko Bolumbu, ameambia waandishi wa habari kuwa ameagiza maafisa wa Msalaba Mwekundu kuelekea huko na kuanzisha juhudi za kutoa misaada kwa watu kwenye eneo la tukio huku shughuli za kutafuta wale ambao hawajulikani waliko zikiendelea.
Comments
No comments Yet
Comment